KAMATI YA SIASA YA MKOA WA GEITA - HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA CHATO

Posted on: November 25th, 2020

Kamati ya siasa ya mkoa wa Geita imepongeza uamuzi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuamua kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda iliyopo Chato na wameshauri jitihada mbalimbali za kuitangaza hospitali hiyo zifanyike ili wananchi waweze kuifahamu na kwenda kupata huduma za matibabu hospitalini hapo.

Hayo yamesemwa leo tarehe 15 Januari 2022 na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Geita ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Mhe. Said Kalidushi na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM Wilayani hapa.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Mhe. Said Kalidushi amesema kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika hospitali hii ni muda muafaka sasa wa wananchi kuifahamu na kufika hospitalini hapa ili kuweza kupatiwa huduma mbalimbali za matibabu badala ya kwenda nje ya nchi ambapo hospitali hiyo hivi sasa imeanza kutoa matibabu kwa wagojwa wa nje.

"Hebu tuitangaze hospitali hii wananchi wote wajue ikoje, hospitali kwa sasa ipo vizuri sana si lazima sana uende hospitali zingine wakati hapa kuna huduma nzuri tena ambazo zamani tulizifuata nje ya nchi" alisema mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule amesema kazi nzuri inayofanywa katika hospitali CZRH ni kutokana na Serikali kutoa fedha kwa wakati ambapo pia amewapongeza wakala wa majengo Tanzania (TBA) kwa kusimamia vyema ujenzi huo.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.