HUDUMA YA KINYWA NA MENO IKITOLEWA NA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO KWA WANAFUNZI WA WILAYA YA CHATO

Posted on: March 20th, 2022

Madaktari wanaohusika na kinywa na meno hospitali ya rufaa ya kanda chato wakitoa huduma na elimu ya kinywa na meno kwa wanafunzi baadhi Wilayani Chato. madaktari hao walisisitiza kuwa Magonjwa ya Kinywa na Meno yana uhusiano mkubwa na mtindo wa maisha au tabia ya jamii husika na hivyo yanaweza kudhibitiwa kwa kubadilisha mtindo wa maisha. Asilimia kubwa ya magonjwa ya meno huchangiwa na ulaji wa vyakula vya sukari kwa wingi na tabia ya kutopiga mswaki kwa usahihi. Ili jamii iweze kubadili tabia, ni vyema elimu ya afya ya kinywa na meno iwe ni mkakati muhimu sana ili magonjwa ya kinywa na meno yaweze kuzuiwa. Makundi muhimu na ya kipaumbele katika kupata elimu hii ni yale yanayofika katika kliniki za kawaida, kliniki za Afya ya Uzazi na Watoto, Wanafunzi wa shule za msingi za kawaida na shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum. Makundi haya yakifikiwa mara kwa mara na kupata elimu stahiki juu ya afya ya kinywa na meno, sehemu kubwa ya jamii inaweza kubadili tabia na mtindo wa maisha hususani juu ya ulaji wa vyakula usiofaa na upigaji sahihi wa mswaki.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.