MAFUNZO YA MFUMO WA UTUNZAJI MALI ZA SERIKALI (GAMIS)

Posted on: August 23rd, 2023

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato wamepata mafunzo ya matumizi ya mfumo wa utunzaji mali za Serikali (GAMIS).Mafunzo haya yatakayodumu kwa siku nne, ambapo Maafisa manunuzi,Wahasibu,Wafamasia,Afisa TEHAMA na Viongozi wananolewa kwa lengo la kuifikia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inayolenga kuendana na uchumi wa kidigitali ,ambapo Serikali iliamua kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mali ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto zilizopo.

Akizungumza katika mafunzo haya,Mhakiki Mali Mkoa wa Geita Ndugu. Adamu Msonde amesema "Hii kama Taasisi ya kiserikali,mfumo huu unaenda kuwezesha kuingiza na kuhuisha taarifa za mali kwenye mfumo kwa wakati,kusimamia mfumo wa GAMIS,uondoshwaji wa mali na kuhakiki taarifa za mali hizo kabla ya kufunga hesabu kama ilivyoelekezwa katika mwongozo wa usimamizi wa mali wa mwaka 2019.

Mwisho,amesisitiza matumizi ya mfumo huu kwa usahihi hususani moduli mama za usajili wa mali na moduli nyingine zilizopo katika mfumo ambapo taarifa hizi zitaiwezesha Serikali kutambua kiasi,idadi,hali na mali zilizopo pamoja na kuiwezesha taasisi kufunga hesabu za kifedha kwa kutumia taarifa zilizowekwa katika mfumo huu wa GAMIS.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.