WANANCHI WAPATA HUDUMA ZA UPIMAJI WA AFYA BURE KATIKA TAMASHA LA UTALII LILILOFANYIKA KATIKA WILAYA YA CHATO

Posted on: November 29th, 2023

Wataalamu na Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato, wameendelea kutoa huduma za afya ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi wa viashiria mbalimbali vya magonjwa yasiyoambukizwa, upimaji wa maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi (HIV/AIDS), huduma ya kumwona daktari kwa ajili ya ushauri wa namna bora na salama ya kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na elimu ya lishe.

Ni katika tamasha la utalii linalofanyika Wilayani Chato, maeneo ya uwanja wa Magufuli ambapo Wananchi wamejitokeza na kupima Afya zao huku wengi wakishukuru kwa huduma hizi kutolewa bure katika tamasha hili.

Tamasha hili la utalii festival @chatoutaliifestival_2023 ambalo limeanza tarehe 26 Novemba huku likitarajiwa kuhitimishwa ifikapo 3 Desemba, 2023, limepambwa na michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mashindano ya uendeshaji baiskeli, uendeshaji mitumbwi (upigaji kasia), lakini pia kutakuwa na mbio za marathoni pamoja na mchezo wa mpira ikiwa ni sehemu pia ya mazoezi na kuimarisha afya.Kauli mbiu ya tamasha hili ni *Utalii ni Uchumi".

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.