TIBA YA KINYWA NA MENO
Posted on: November 19th, 2020Matatizo ya meno ni shida au magonjwa yanayohusiana na meno, karibia matatizo yote ya meno yanatokea baada ya bakteria na wadudu wengine kuwepo mdomoni, hii hufanya mtu kuwa na maumivu makali kwenye meno na mpaka kupelekea kutoa damu au halufu mbaya na kuathiri meno. Matatizo mengi ya meno yanazuirika na hutibika.
AINA ZA MAGONJWA YA MENO
Mdomo una magonjwa mengi ila meno ndio tatizo kubwa sana na ndio linaweza kuleta na matatizo mengine, aina za magonjwa ni kama;
Meno kutoboka –
Meno kuvunjika –
Meno kusagika au kupungua kimo
Tatizo la fizi
Meno kuharibika, fizi kuachia na kulegea.
Meno kufa ganzi na kushindwa kuhisi
Mhozo au Utando mdomoni
Meno kuwa na rangi ya njano, kaki au kahawia
