ZAIDI YA WANANCHI 800 WAMEPATA HUDUMA ZA KIBINGWA ZA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO BURE KATIKA MAONESHO YA SABA YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI MJINI GEITA.

Posted on: October 13th, 2024



13 OKTOBA, 2024
EPZA BOMBA MBILI, GEITA.

Ikiwa ni siku ya kumi na mbili (12) tangu kuanza kwa maonesho ya kimataifa ya saba ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bomba mbili mjini Geita, zaidi ya wananchi 800 wamehudumiwa katika banda la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) tulioshirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika utoaji huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo hadi leo Oktoba 13 2024.

Kati yao wananchi waliohudumiwa, 457 walikuwa wanawake sawa na asilimia 53% na 399 walikuwa wanaume sawa na asilimia 47%. Watoto 11 wamegundulika kuwa na magonjwa ya moyo na wamepewa rufaa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Copyright ©2022 CHATOZRH . All rights reserved.